Badilisha lugha English
Mwanzo Kuhusu Ensol Huduma zetu Bidhaa Miradi Maktaba ya picha webmail Habari na matukio Wasiliana nasi
Questions about solar?
Request a quote
What type of installation are you interested in?

Home »About us »Kuhusu Ensol

KUHUSU ENSOL

Ikiwa imeanzishwa mnamo Agosti, 2001, ENSOL (T) LTD ni kampuni ya Kitanzania kwa asilimia 100. Kampuni hii imesajiliwa kwenye Bodi ya Usajili wa Makandarasi kama Mkandarasi wa Umeme mwenye kumakinikia Nishati ya Jua. Kampuni pia ni mwanachama mshirika wa Chama cha Nishati ya Jua Tanzania ambacho kinajumuisha makampuni yote ya Nishati Ijizalishayo. 

ENSOL (T) LTD ina wakurugenzi uzoefu na utaalamu kubwa na mpana katika Nishati Ijizalishayo na katika shughuli za kibiashara kwa jumla. Tunao pia wafanyakazi wenye sifa na uzoefu na wenye kumakinikia bidhaa tunazojishughulisha nazo ambazo zimepitia majaribio makali katika maabara yanayotambuliwa kimataifa. Twasifika pia kama wagavi wa bidhaa za nishati ya jua za ubora wa hali ya juu; na kwa kila mradi wa nishati ya jua unaofungwa tunatoa msaada wa kiufundi wa kiwango cha juu.

Rajua(mission)
Tunaazimia kuwa wagavi wa kuaminika kabisa wa huduma za nishati ya ubora wa juu, nafuu na safi. 

Dango(Vision)
Kuwa chaguo la kwanza la wateja katika utoaji wa huduma za nishati safi nchini Tanzania

Amali
1.    Hehima kwa uhai na mazingira
2.    Kusikiliza na kujifunza kutoka kwa wateja na washirika wetu
3.    Kukamia kuwa wavumbuzi
4.    Kukamia kufanya kazi kama timu wakati wote
5.    Kuwaridhisha wateja
6.    Kuitikia mahitaji ya wateja

Shabaha
Kuongoza katika kutoa kwa urahisi na kwa bei nafuu bidhaa na huduma bora za nishati safi

MKABALA WETU
Kwanza, tunalenga kuelewa mahitaji yako, kisha tunakushauri kwa msingi wa uzoefu wetu mpana, tunabuni mfumo na kumwasilishia mteja makadirio sahihi. Ikiwa una mahitaji pungufu au zaidi katika mfumo wako, hilo si tatizo kwetu; tunatafakari maombi yako ili kukidhi mahitaji yako yote.
Katika ENSOL (T), pia tunatoa:

 Mafunzo — kumwezesha yeyote kuamua kama awekeze katika nishati ya jua au la na pia kama njia ya kutoa taarifa ya kuaminika kuhusu mifumo ya nishati ya jua.
Ubunifu wa mfumo — kwa ajili ya mahitaji yako ya nishati kama mtumiaji wa kudumu au wa muda katika makazi yako, mahali pa biashara au popote pale.

Huduma ya pekee — tunakupa huduma huduma bora kabla, wakati na baada ya ufungaji kwa kuzingatia mambo yote muhimu na kwa kufuatilia kwa karibu utendaji wa mfumo wako wa nguvu za jua hapo baadaye.
Tegemeo la hakika — tunahakikisha kuwa mfumo wako unakidhi viwango vya juu kabisa vya ubora na kuaminika.

Mafanikio
Mafanikio yetu yanayotufurahisha sana ni ule uwezo wetu wa kusambaza nguvu ya nishati ya jua kwa mamia ya wakazi wa maeneo ya vijijini nchini Tanzania. Leo hii, idadi kubwa ya kaya, zahanati, vituo vya afya, hosipitali, shule, vituo vya kuwalea yatima, Mbuga za Taifa, Mbuga za wanyama na ofisi zilizo mbali na gridi ya taifa zinafurahia umeme wa jua tunaousambaza.

ENSOL pia imeshiriki katika shughuli nyingine mbalimbali kitaifa na kimataifa. Kitaifa, tumeshiriki katika Maonyesho ya Biashara ya Taifa nchini Tanzania kwa mafanikio makubwa. Kwa mfano, katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ya 32 mnamo 2007 tulikuwa washindi wa pili katika Kundi la Vifaa vya Elektroniki na katika maonyesho hayo ya 33 mnamo 2008, ENSOL ilipata zawadi ya pili katika kundi hilo. Kimataifa, ENSOL, mnamo 2008, ilishiriki katika Mashindano ya Benki ya Dunia ya Uendelezaji wa Soko la Kuiangaza Afrika na kuwa miongoni mwa washindi 54. Yakiwa na dhamira inayofanana na rajua yetu, mashindano hayo yaliwavutia mamia ya washiriki kote duniani.

ENSOL pia imefungua tawi lake la kwanza huko wilayani Karatu mnamo Oktoba 2008 kuhudumia maeneo ya mikoa ya Arusha na Manyara.

There have been 3217 visitors to this websiteThere have been 3217 visitors to this websiteThere have been 3217 visitors to this websiteThere have been 3217 visitors to this website
User online : 1
Copyrights ©2009 Ensol (T), All Rights Reserved