Badilisha lugha English
Mwanzo Kuhusu Ensol Huduma zetu Bidhaa Miradi Maktaba ya picha webmail Habari na matukio Wasiliana nasi
Questions about solar?
Request a quote
What type of installation are you interested in?

Home »Products »Bidhaa za ensol

BIDHAA
ENSOL (T) Ltd inafanya kazi kwa karibu na wauzaji maarufu wa kimataifa wa bidhaa za nishati ya jua na imeweza kuwapa wateja wake bidhaa na huduma za kisasa kabisa na za hatua ya juu kiufundi.

Tumeteua bidhaa na wagavi wetu kwa namna kwamba bidhaa za ubora  na zilizofanyiwa majaribio kwenye maabara yanayotambuliwa kimataifa na kupita viwango vya ubora vya kimataifa tu ndizo hutumika katika miradi yetu.

Kwa jumla, tunasambaza vifaa na mifumo iliyokamilika kwa ajili ya umeme wa nishati ya jua, huduma saidizi and vichemsha maji vya nguvu za jua.

1. Mifumo ya umeme wa nguvu za jua

Nishati ya jua imeanza kuenea, na watu duniani kote sasa wameanza kutumia teknolojia tofautitofauti kupata zawadi hii kutoka maumbile ya asili.

Mfumo wa umeme wa nguvu za jua ndio hupendelewa zaidi kama njia ya kukabili mahitaji ya kawaida kama kupata mwanga na kuendesha vifaa kama radio, televisheni, kompyuta,radio za  Vhf & Hf, vituo vya mawasiliano, na kadhalika, hasa katika maeneo umeme wa gridi usipopatikana au usipokuwa wa kuaminika.


Paneli za Jua

Paneli ya jua ndicho kiini cha mfumo wowote wa umeme wa jua. Imebuniwa kwa namna kwamba pale inapopigwa na miwanga wa jua inazalisha umeme.

Tunasambaza aina tofautitofauti maarufu kama vile Kyocera, Sharp lakini aina inayopendelewa zaidi ni Suntech, kutoka kampuni ya Suntech Power Co. Ltd, ambayo ilikuwa mtengenezaji mkubwa wa tatu duniani mnamo 2008.

Betri za Nishati ya jua (Tangi la nishati ya umeme)


Wakati paneli za jua zikizalisha umeme zinapopigwa na mwanga wa jua, zenyewe haziwezi kuhifadhi umeme huo. Hivyo, betri ndio hupokea na kuhifadhi umeme uliozalishwa na paneli za jua kwa ajili ya matumizi ya baadaye (usiku au siku mawingu yanapotanda). 

Tuna aina aina tofautitofauti za teknolojia za betri oevu na kavu. Hata hivyo, aina zilizo maarufu zaidi ni Deka & Victron (kwa aina kavu) na Surrette (kwa aina oevu). Pia tunatumia betri za nishati ya jua zilizorekebishwa kwa ajili ya mifumo midogo ya umeme wa jua kwa matumizi ya nyumbani.

Kidhibiti Nishati ya Jua

Paneli ya jua haijawekewa utaratibu wa kugundua kama betri imejaa na wala betri haijatengenezewa uwezo wa kukata umeme kutoka kwenye paneli pale inapojaa. Matatizo haya mawili yanafanyiwa kazi na chombo kinachojulikana kama kidhibiti nishati ya jua. Hiki ni chombo kinachozuia betri isijazwe umeme kupita kiasi na paneli au isipate umeme pungufu. Chombo hiki kinatumika pia kufuatilia mfumo hadi kwa mtumiaji.

Aina maarufu za vidhibiti nishati ya jua tulivyo navyo vinatoka kampuni ya Morningstar ya Marekani na aina nyinginezo kutoka makampuni ya Steca na Phocos ya Ujerumani.

Vigeuza umemejua
Umememe unaotumiwa majumbani na katika sehemu za kazi ni wa aina ya mkondogeu wakati paneli za jua huzalisha umeme wa aina ya mkondofulizo. Hivyo, bateri za umeme wa jua huhifadhi na kutoa umeme wa aina ya mkonofulizo. Ili umeme umeme wa aina ya mkondofulizo uweze kubadilishwa kuwa wa aina ya mkondogeu, kunahitajika chombo kinachojulikana kama kigeuza umemejua. Vigeuza umemejua ni vyombo vya kugeuza umeme wa aina ya mkondofulizo kwa umeme wa aina ya mkondogeu katika volteji na mirudio ya kawaida ili ziweze kutumika kuendesha umeme wa mikondogeu.
ENSOL (T) Ltd ina vigeuza umemejua na vilevile na chaja za vigeuza umemejua kutoka kampuni ya Xantrex Technology ya Marekani, kampuni ya Victron Energy B.V ya Uholanzi na kampuni ya Outback Power ya Marekani.

Taa za umemejua
ENSOL (T) Ltd inazo na inauza taa zenye uhai wa zaidi ya saa 8000 na vilevile taa za LED zenye uhai wa zaidi ya saa 100,000 kutoka kampuni ya Phocos ya Ujerumani. Aina ya taa inayopendelewa zaidi ni Sundaya ambazo ni za balbu za kawaida. Aina nyingine ya taa zinazopatikana ni Magnaray inayotumika katika mifumo ya taa za barabarani.

Pamoja na vyombo hivi vikuu vya umeme wa jua ni vingne kama vile vya kutundikia vifaa vinavyotumika kuweka paneli za jua na vifaa vya kuunganishia na vitu kama kebo, swichi, soketi, na kadhalika.

2. Mifumo ya Betri Saidizi

Vifaa vya majumbani na maofisini na vifaa kama vile kompyuta, faksi, taa, baruapepe, simu, mafriji, televisheni, na kadhalika, hufanya kazi vizuru na kwa usalama pale umeme unapokuwa endelevu na wa kuaminika. Hali hii huwa inahakikishwa na mifumo ya betri saidizi.

 Mifumo ya betri saidizi huwekwa kwa namna kwamba umeme wa gridi unapokatika, hii mifumo hujiwasha yenyewe na kuendelea kutoa umeme kwa muda kutegemea uwezo wa mfumo na ukubwa na nguvu ya betri. Pale umeme wa gridi unaporudi, mfumo wa betri saidizi huwasha vifaa kurjea kwenye umeme wa grid, huchaji betri yake na kukaa tayari kusubiri umeme kukatika.

ENSOL (T) Ltd inatoa mifumo ya betri saidizi yenye sifa zifuatazo:

  • Nguvu saidizi ya papohapo
  • Hujiendesha yenyewe
  • Imekingwa isipate umeme kupita kiasi
  • Volteji hujdhibiti yenyewe
  • Haina kelele wala moshi
  • Haitumii fueli mara ifungwapo
  • Hutoa nguvu nyingi
  • Hujiendesha bila kikomo
  • Ni ya kuaminika kabisa, na kadhalika

Kuamua ukubwa wa mfumo wa betri saidizi unaohitajika kunategemea idadi ya vifaa vinavyotumika, nguvu zake na  muda wa umeme kukatika. Tuna aina tofautitofauti za vifaa vya mifumo saidizi zinazofaa kwa mahitaji yako ya umeme kwa mkondo mmoja au mikondo mitatu. ENSOL (T) Ltd inasanifu mfumo wa betri saidizi yenye kulingana na nguvu ya umeme kwa ajili bei haliisi na uhai.

3. Mifumo ya Vichemsha maji vya umemejua

Mifumo ya vichemsha maji vya umemejua huhudumia kaya, hoteli, zahanati, hosipitali, mabweni, na kadhalika, kwa maji ya moto yasiyokatika. Ingawa gharama za mwanzo za ununuzi na ufungaji wa mifumo hii ni za juu ukilinganisha na zile za gesi au umeme, zinapunguza sana gharama za umemes; na unavyoitumia kwa wingi, ndivyo unavyookoa umeme kutegemea ulipo na hali ya hewa. Mfumo wa vichemsha maji vya umemejua pia hupunguza sana joto inayoathiri mazingira. 
ENSOL (T) LTD inasambaza na kufunga aina tofautitofauti za mifumo kamili za vichemsha maji vya umemejua kutoka kampuni ya MEGASUN ya Ugiriki na kampuni ya CHROMAGEN ya Israel kwa bei nafuu sana.

There have been 3216 visitors to this websiteThere have been 3216 visitors to this websiteThere have been 3216 visitors to this websiteThere have been 3216 visitors to this website
User online : 1
Copyrights ©2009 Ensol (T), All Rights Reserved