|
HUDUMA
ENSOL (T) Ltd inajihusisha na ubunifu, ugavi na ufungaji wa mifumo ya kuaminika ya nguvu za jua na vichemsha maji vinavyotumia nguvu za jua kwenye kaya, Asasi za Serikali na za Kidini, Mashirika ya Kimataifa ya Misaada, makampuni binafsi, na kadhalika, ikitumia paneli za nishati ya jua na vifaa vyenye kuhusiana nazo za ubora wa juu kabisa.
Kubuni & Kupanga kwa saizi
Uangalifu mkubwa unachukuliwa tunapobuni mfumo wako wa nguvu ya jua kwa ajili ya matumizi nyumbani kwako, mahali pa biashara au popote pale kuhakikisha usalama na uimara. Kuhusu usalama, vyanzo na saketi zote za umeme zinawekewa fyuzi, vikata umeme ipasavyo. Na uimara unahakikishwa kwa matumizi ya vifaa bora na visivyowasumbua watumiaji.
Ufungaji
Ufungaji unafanyika kulingana na maelekezo na kwa kuzingatia maadili ya uendeshaji wa mitambo ya umeme. Kampuni pia ina karakana yenye kompyuta iliyounganishwa kwenye intaneti kwa ajili ya uigaji na ufuatiliaji wa mifumo na inayotumiwa kuchora vielelezo mbalimbali. Karakana pia ina vifaa vya majaribio na upimaji (kama vile mita za AVO, Haidromita, umeme, n.k.) na vyombo vya kufanyia kazi (kama vile keeke za mkono za mikondo badilifu na mikondo ya moja kwa moja, keekee gandamizi, nyundo ya kulehemia, n.k.).
Huduma saidizi (Huduma baada ya mauzo)
Kwanza kabisa, vifaa vyote vikuu vya nguvu za jua tunavyosambaza vina hati za watengenezaji na, pili, kampuni inafanya matengenezo ya bure kwa mwaka mzima baada ya kufikishwa, kufungwa na kuanza kazi. Katika kipindi hicho majukumu yetu ni:
- Kuifanyia majaribio mifumo ya umeme wa nguvu za jua
- Kufanya matengenezo ya kawaida
- Kujadili utendaji na matumizi ya mifumo hiyo na wafanyakazi husika
- Kuendelea kuwapa mafunzo wale wanaotunza na kuendesha mifumo hiyo.
Kwa jumla, wateja wanapata sio tu bidhaa za ubora wa juu kwa bei nafuu bali pia huduma za kitaalamu,huduma za kiufundi za baada ya mauzo, ushauri wa bure, dhamana na kufikisha bidhaa bila gharama kwa jiji la Dar es Salaam. |